Kuna
ishu ya jinsia ya mtoto anaezaliwa, kati ya wazazi huenda ikatokea kati
yao akawepo mmoja ambae anatamani kuwa na mtoto wa kike na mwingine
akawa anatamani awe na mtoto wa kiume..
Rameshwar Rao aliamua
kumfungia mkewe na mtoto wake wa kike bafuni kwa muda wa miaka mitatu
kisa tu mwanamke huyo amejifungua mtoto wa kike wakati mwanaume alikuwa
anahitaji kuwa na mtoto wa kiume.
Baada ya mkewe Priyanka kugundua
ni mjamzito wa mtoto wa kike alimwambia mumewe ambaye alimtaka aitoe
mimba kwa kuwa alitaka mtoto wa kiume, lakini mkewe alikataa kuitoa na
kuamua kurudi kwa wazazi wake akajifungue.
Mwanamke
huyo alitaka kukimbia baada ya kujifungua, mwanaume akaamua kumkamata
na kumfungia kwenye choo pamoja na mtoto wao wa kike kwa muda wa miaka
mitatu huku akiwa anawapa wali na maji kwenye bakuli kila siku.
Kwa
sasa mwanaume huyo anashikiliwa na polisi baada ya marafiki wa familia
yake kugundua kitendo alichokifanya kwa mkewe lakini mke wake amewaomba
polisi hao kumwachia huru ili waendelee kuishi pamoja.
