Marry Alia na Rushwa ya Ngono Bongo Movie

Marry Alia na Rushwa ya Ngono Bongo Movie
MERRY MSANII BONGO MOVIE
              
 MSANII chipukizi wa filamu Marry Elias amewalalamikia baadhi ya watengeneza filamu kwa kuwanyanyasa na kuwadhalilisha wasanii chipukizi kwa kuwaomba rushwa ya ngono, msanii huyo anasema kuwa wasanii wasio majina ambao wanapofika katika usahili wa filamu ukwama hadi watoe rushwa ya ngono.
“Katika tasnia ya filamu Bongo kwa mtoto wa kike kuna changamoto nyingi lakini inayoniumiza ni baadhi ya wasanii kututaka kimapenzi ndio akupe kazi yake au anaweza asikupe kabisa na hiyo, ni vizuri kuangalia uwezo wa muigizaji na si rushwa ya aina yoyote ile,”anasema Marry.
Msanii huyo anasema kuwa kuna baadhi ya wasanii wakubwa kabisa ambao pamoja na kuwa hawana sinema lakini uandaa muswada (Script) na kuwaita wasanii nyumba za kulala wageni, wakiahidi kuwapatia kazi lakini wakifanikisha mambo yao hakuna filamu tena wala kazi

wdcfawqafwef