MSANII WA BONGO MOVIE ATANGAZA KUGOMBEA UBUNGE MBEYA MJINI KWA TIKETI YA CCM


Waandishi wetu
KUMEKUCHA! Nyota wa sinema za Kibongo, Jimmy Mafufu ameibuka na kuwa msanii wa kwanza kutangaza nia ya kugombea ubunge wa Jimbo la Mbeya Mjini kwa ‘leseni’ ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Nyota wa sinema za Kibongo, Jimmy Mafufu.
Akipiga stori na safu hii juzi jijini Dar, Mafufu alisema amefikia uamuzi huo baada ya kuombwa na wananchi wa jimbo hilo kwa vile mbunge wa sasa, Mheshimiwa Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) hajatimiza ahadi zake.



“Nakwenda Mbeya, Ijumaa (Leo) nitatua kwenye Uwanja wa Ndege wa Songwe, nitapokelewa pale na wana-CCM tayari kwa kuanza mchakato wa kuchukua fomu kwa tiketi ya CCM kugombea ubunge. Ni mimi tu ndiye nitakayeiweza Mbeya Mjini,” alisema Mafufu.
CHANZO  EDDY BLOG

wdcfawqafwef