Kilimanjaro Stars karata muhimu leo

kocha mkuu wa kilimanjaro stars Abdallah Kibaden



TIMU ya soka ya Taifa ya Bara, Kilimanjaro Stars leo itarusha karata yake ya pili kwenye michuano ya Kombe la Chalenji itakapomenyana na Rwanda ‘Amavubi’ mjini Awassa, Ethiopia.
Mechi hiyo inatarajia kuwa ya vuta nikuvute kutokana na Tanzania na Rwanda kuwa timu zenye ushindani mkubwa katika soka ya ukanda wa Mashariki na Kati na hasa kwenye michuano hiyo. Kila timu inaingia uwanjani ikitoka kushinda mechi yake ya kwanza, jambo linalozidi kufanya ugumu katika mechi hiyo na kuwa isiyotabirika.
Kili Stars ilifanya‘mauaji’ katika mechi ya kwanza baada ya kuishushia kipondo cha mabao 4-0 Somalia mwishoni mwa wiki iliyopita, huku Rwanda ikipata ushindi wa kushtua kwa kuwafunga wenyeji Ethiopia bao 1-0 katika mechi ya ufunguzi. Ushindi kwa kila timu katika mechi ya leo ni muhimu ili kujihakikishia nafasi ya kutinga hatua ya robo fainali.
Kwa mujibu wa kanuni za michuano hiyo, timu mbili za juu kutoka kila kundi kati ya makundi matatu zitafuzu robo fainali pamoja na timu mbili zilizoshika nafasi ya tatu kwa uwiano mzuri ‘bestloser’ na kufanya idadi ya timu nane zitakazocheza robo fainali.
Katika kundi A mpaka sasa Kili Stars na Amavubi zipo kwenye nafasi nzuri baada ya kushinda mechi zao za kwanza. Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya mtandao nahodha wa Kili Stars, John Bocco alisema hana shaka na kupata matokeo mazuri leo.
Alisema baada ya mechi dhidi ya Somalia timu yake imeimarika zaidi na morali yao iko juu kutaka ushindi. “Morali yetu iko juu kwa sasa tumeshasahau matokeo mabaya yaliyopita na sasa tunataka kushinda kwenye Kombe la Chalenji… baada ya mechi na Somalia timu yetu ipo vizuri sana,” alisem

wdcfawqafwef