Hali mbaya! Lile bifu la
waigizaji wa filamu za Kibongo, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ na Kulwa
Kikumba ‘Dude’ limefika pabaya ambapo wamekuwa wakitoleana maneno
makali kwamba mmoja wao akifa hawatazikana.
Stive Nyerere.
Chanzo cha wasanii hao
kugombana kilitokana na kaburi la marehemu Adam Kuambiana ambalo
limejengwa hivi karibuni ambapo kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram,
Steve Nyerere aliandika waraka mrefu akiwashutumu Dude na William Mtitu
kwamba wao ndiyo wanaomchafua.
Kulwa Kikumba ‘Dude’
Akieleza hali ilivyo kwa
sasa, Dude alikuwa na haya ya kusema: “Unajua kusema kwangu ukweli
ndiyo unanigombanisha na Bongo Muvi. Pamoja na jitihada za kupatanishwa,
Steve amekataa na amesesema hata nikifa hawezi kuja kunizika.”
Kwa upande wa Steve naye alisema: “Huyo Dude aendelee na maisha yake.”

