Kutoka kwenye mtima! Staa wa Bongo Fleva, Zuwena Mohamed ‘Shilole’
amefungukia ishu ya kumbebea mimba mpenzi wake, Naftal Mlawa ‘Nuh
Mziwanda’ ili kuwafunga midomo wanawake wa mjini ambao wanamzengea jamaa
huyo.
Staa wa Bongo Fleva, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ akiwa katika pozi na mpenzi wake Nuhu Mziwanda.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Shilole alitiriria kuwa, kwa muda mrefu
amekuwa akibanwa na kazi zake za muziki ambazo anafanya na mpenzi wake
huyo kiasi kwamba hawakufikiria kuhusu kupata mtoto mapema.
“Kwa sasa nimepanga kumbebea mimba na kumzalia Nuh,” alisema Shilole au Shishi Baby.
