Shamsa Ford anamlea mtoto wa Nay Wa Mitego?

Shamsa Ford anamlea mtoto wa Nay Wa Mitego?
shamsa
Picha iliyosambaa mtandaoni ikimuonyesha mwigizaji wa filamu za Kibongo,Shamsa Ford akiwa amembeba mtoto wa staa wa Bongo Fleva,Nay Wa Mitego,Curtis imezua maswali kwa mashabiki wao kuwa huenda mwigizaji huyo kwa sasa anamlea mtoto huyo .
shamsa1
Miezi ya hivi karibuni Nay Wa Mitego aliamua kumchukua mtoto wake kutoka kwa mama yake Siwema aliyekuwa akiishi jijini Mwanza baada ya kutoelewana kati yao na minong’ono ilisambaa kuwa msanii huyo anatoka kimapenzi na Shamsa Ford.
nay
Hata hivyo wote wawili walikana kutoka kimapenzi na kwamba ni marafiki wa kawaida,Clouds Fm imezungumza na Nay kuhusu picha hiyo alisema kuwa mwigizaji huyo ni rafiki wa dada yake alienda kumtembelea na kumbeba mtoto huyo na kupiga naye picha.
‘’Siyo kweli kwamba mtoto wangu analelewa na Shamsa namlea mwenyewe na mama yangu alienda kumtembelea dada yangu akapiga picha na Curtis,’alisema Nay.

wdcfawqafwef