Mama Kanumba, Mama Lulu Kimenuka!

Mama Kanumba, Mama Lulu Kimenuka!
     


    Taarifa zilizolipotiwa na gazeti la ijumaa zinadai kuwa, wale wamama wa mjini ambao walikuwa mashosti hadi kufikia hatua ya kusema ni kama ndugu, mama wa aliyekuwa staa wa Bongo Movies, marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa na mama wa mwigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’, Lucresia Karugila, sasa kimenuka!
    Chanzo cha gazeti hilo cha kuaminika kilidai kuwa, dalili za wawili hao kuelekea kugeuka kuwa paka na chui zilianza muda mrefu lakini hali ikazidi kuwa mbaya Siku ya Kumbukumbu ya Kifo cha Kanumba, Aprili 7, mwaka huu alipokuwa akitimiza miaka mitatu kaburini.
    Ubuyu ulidai kwamba, siku ya kumbukumbu ya kifo cha Kunumba, Mama Kanumba alimtuhumu Lulu kutotoa ushirikiano na kufikia hatua ya kutoa maneno makali zaidi yaliyomkera mama Lulu.
    Ilizidi kudaiwa kwamba, wakati mama Lulu akitafakari sababu ya shosti wake huyo ambaye walikuwa wakitembea mjini kama kumbikumbi kumtumia sms hiyo, akashangaa kusoma tena kwenye gazeti mama Kanumba akimpa vipande vyake Lulu, jambo lililozidi kumchefua mama Lulu.
    “Kimsingi hali ni mbaya sana sasa hivi, inavyoonekana mama Lulu kamchoka mama Kanumba na anataka kuchukua hatua zaidi ikiwemo kuburuzana kortini,” alidai sosi huyo.
    Baada ya kunyetishiwa ishu hiyo, gazeti hilo lilimtafuta mama Lulu ambapo alipopatikana alikiri kupokea ujumbe na kwamba hali ni mbaya sana.“Nimeumizwa sana na sms ya mama Kanumba lakini siwezi kuwapa kwa sababu nataka kuifanyia kazi,” alisema mama Lulu.
    Kwa upande wake mama Kanumba aliendelea kusisitiza kuwa yeye ataendelea kumlilia mwanaye na hana mpango na familia hiyo ya Lulu.“Mimi kwa upande wangu nitamlilia mtoto wangu mpaka siku ya kufa kwangu lakini kinachoniuma ni Lulu kufanya sherehe ya mdogo wake siku ya kumbukumbu ya mwanangu.
    “Jamani hata kama mtu ana roho gani, hawezi kufanya hivyo,” alisema.
    Alipoulizwa kuhusu sms aliyomtumia mama Lulu na kwamba mama huyo yupo mbioni kumchukulia hatua za kisheria hakuwa tayari kuzungumza chochote.

    wdcfawqafwef