Explosion DAR

Watu kadhaa wauawa kwenye mlipuko Dar
17 Februari 2011 02:52
Hali ya taharuki imetanda mji wa Dar Es Salaam, nchini Tanzania, huku wakaazi wakiamka kuomboleza vifo vya zaidi ya watukumi na zaidi ya wengine 60 kujeruhiwa kufuatia milipuko iliyotokea kwenye ghala la kuhifadhi silaha za kijeshi, lililo karibu na uwanja wa kimataifa wandege.
Wakaazi wa eneo la Gongo la Mboto lililo karibu na ghala hilo wamekesha nje baada ya makaaziyao kubomoka kutokana na mtikisiko wa milipuko hiyo iliyodumu kwa saa kadhaa. Milipuko hiyo ilisikika kwa umbali wa zaidi ya kilomita ishirini kutokakituo hicho cha kijeshi.
Inaarifiwa kuwa milipuko hiyo ilianza mwendo wa saa mbili usiku.
Msemaji mmoja wa jeshi amesema kuwa kuna watu wengi ambao wamepoteza maisha yao lakini idadi kamili haijajulikana.
Kamanda wa polisi jijini Dar-es-Salaam, Suleiman Kova, ametoa wito kwa raia wa mji kuwa huo watulivu huku maafisa wa ulinzi wakiendelea na mikakati ya kurejesha hali ya uthabiti.
Kova amesema uchunguzi wa awaliumebainisha kuwa mlipuko huo ni ajali na wala sio shambulio la kigaidi.
Ni hii mara ya pili kwa milipuko kama hiyo kutoka jijini Dar es Saalam katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.
mwaka wa 2009 zaidi ya watu ishirini waliuawa na wengine 300 kujerihiwa

wdcfawqafwef